The House of Favourite Newspapers

Aucho: Nimezoea Mechi Ngumu

0

KIUNGO mkabaji wa Yanga, Mganda, Khalid Aucho, amefichua kuwa kwake haikuwa shida kufanya vizuri katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba kwa kuwa amezoea kucheza mechi ngumu bila ya kuwa na presha.

 

Wikiendi iliopita, kiungo huyo alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Yanga baada ya kujiunga na timu hiyo msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea El Makasa ya Misri.

 

Katika mchezo huo wa Ngao ya Jamii ambao ulipigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Aucho alisema: “Binafsi kwangu imekuwa ni furaha kubwa kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii, hii ni zawadi yetu kwa mashabiki ambao wamekuwa wakituunga mkono. Ukiangalia hatukufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo sikucheza.

 

“Huu mchezo kwangu haukuwa mgumu na sijaona ugumu wowote kwa sababu nimezoea kucheza mechi za namna hii. Tunaenda kuanza ligi ambayo ni ndefu na ngumu, lakini malengo na matumaini yetu ni makubwa.”

~~Ibrahim Mussa, Dar

Leave A Reply