The House of Favourite Newspapers

Yanga: Tuna Ukuta wa Chuma

0

UONGOZI wa Yanga umebainisha kwamba umesajili wachezaji chuma jambo ambalo linawafanya wawe na ukuta mgumu kama wa Berlin huku eneo la viungo likiwa imara pia.

 

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli, aliliambia Spoti Xtra kuwa, dhamira kubwa ya kufanya usajili makini ni kuwa na chaguo la kufanya kwenye kila mechi ili wapate pointi tatu.

 

“Unaona kwamba kwenye mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar eneo la beki wa kati hakuanza Bakari Mwamnyeto ambaye ni nahodha, lakini ilikuwa kama hakuna kilichotokea, kazi ilifanyika na tukapata ushindi. Tuna ukuta kama ule wa Berlin.

 

“Kwa upande wa viungo hakuwepo Tonombe Mukoko kwa sababu alikuwa na adhabu, lakini bado eneo la kiungo lilikuwa imara na kufanya vizuri,” alisema Bumbuli.

 

Naye Msemaji wa Yanga, Haji Manara, alibainisha kuwa: “Unakuwa na mchezaji mwenye uwezo mkubwa kama Bangala (Yannick), unadhani unahitaji nini kingine kama sio ushindi? Yupo yule Khalid Aucho, huyu ni mzee wa pasi za uhakika kuna burudani kweli Yanga.”

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar

Leave A Reply