×

Rosa Ree Amrushia Vijembe Kwa Eksi Wake

BAADA ya kuchumbiwa hivi karibuni, rapa wa kike Bongo, Rosa Ree amemrushia vijembe rapa wa Kenya, Timmy Tdat ambaye aliwahi kudaiwa kutoka naye kimapenzi akisema hakumbuki kama aliwahi kutembea naye.

 

Wawili hao waliwahi kudai ni wapenzi na kila walipokwenda, kila mmoja alimsifia mwenzake kimahaba.

 

Lakini mara tu baada ya kuchumbiwa na jamaa aliyetajwa kwa jina la King Petrousse, Rosa Ree amebadilika kabisa na kusema; “Sijawahi kumtambulisha mwanaume yeyote kama mpenzi wangu, hii ni mara yangu ya kwanza kufanya hivi…”

STORI ZOTE; MWANDISHI WETU, DAR

Leave a Comment