
Jana Oktoba 5, 2021 zimetimia ni siku ya 40 tangu kijana Hamza aliyeuwa askari Dar es Salaam kisha na yeye kuuawa na jeshi la polisi.
Wananchi wa Kitongoji cha Kitete, Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi wilayani Chunya mkoani Mbeya wamemkumbuka kwa kufanya sherehe ndogo ambayo imewajumuisha wanakijiji na watu wa karibu wa Hamza.
Wananchi hao wamekiri kuwa Hamza aliwasaidia mambo mengi ikiwemo ujenzi wa ofisi ya chama na kuchangia katika elimu hivyo watamkumbuka sana.