
TRELA la lori la mizigo lenye namba T165 DVG limewaka moto usiku wa kuamkia leo katika eneo la Ubungo Kibo jijini Dar es Salaam baada ya matairi yake ya nyuma, upande wa kushoto kuwaka moto.
Wananchi mbalimbali wakiwemo Wakazi wa Ubungo Kibo na wapita njia, wamefanikiwa kuuzima moto huo kwa maji, fire extinguisher na mchanga.
Aidha, hakuna madhara ya kujeruhiwa wala vifo vilivyotokea kutokana na moto huo ambao chanzo chake hakikufahamika mara moja.