×

Yamoto kumrudia Godfather

IMG_20150107_010322Yamoto Band.

ANDREW CARLOS
Baada ya kutikisa na Video ya Cheza kwa Madoido,bendi inayotikisa Bongo,Yamoto inatarajia kurudi tena kwa mtayarishaji aliyewaandalia video hiyo, Mike Ogoke ‘Godfather’ kwa ajili ya video yao nyingine itakayotambulika kama Elea.

Meneja wa kundi hilo, Said Fella alisema licha ya hilo, pia kwa mara ya kwanza mashabiki wataisikia nyimbo hiyo Desemba 19, mwaka huu ndani ya Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

“Cha msingi ni kusogea Dar Live Desemba 19, kushuhudia Yamoto wakitambulisha ngoma zao kama vile Imo na Elea ambazo ni kali kuliko zote zilizowahi kutoka.

“Usiku huo pia kwa mara ya kwanza msanii kutoka Mkubwa na Wanawe, Baby J naye tatambulisha ngoma yake mpya na pia tutamtambulisha mshindi wa Bongo Star Search (BSS 2015) Kayumba Juma,” alisema Fella.

Leave a Comment