×

Petit Man: Mama Watoto Wangu Ana Raha

MENEJA wa wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva, Hamad Manungi ‘Petit Man’ amesema kuwa, mama watoto wake wa sasa ana raha mno kwa sababu yeye ni baba ambaye anapenda mno watoto wake hivyo hata usiku mtoto wake Kian akisumbua yeye ndiye anaamka kumbembeleza.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Petit Man alisema kuwa, hakuna kitu anachokipenda kama ulezi wa watoto wake kwa sababu anapenda mno watoto hivyo mwanamke wake hana shida ya kusumbuka na mtoto.

 

Anasema kuwa, mara nyingi yeye akiwa nyumbani ndiye anambeba na kutembea naye huku na kule hivyo anawasihi wababa wengine wawe hivyo na siyo kila kitu wanamwachia mwanamke.

 

“Mimi naamini mama watoto wangu ana raha sana kwa sababu napenda kulea watoto wangu mwenyewe na siyo mvivu kwenye kumbeba mtoto wala kumbembeleza. Nashangaa wababa wengine wavivu, hawawezi hata kubeba mtoto,” anasema Petit Man ambaye pia alikuwa mume wa mwanamama Esma Platnumz kabla ya kutengana na sasa ana mama mtoto mwingine.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave a Comment