
BAADA ya pati ya kusikiliza Albam ya Only One King ya King Kiba kufanyika jijini Dar, wikiendi iliyopita ilikuwa ni zamu ya kusikilizwa nchini Kenya na ndipo msanii huyo akakutana uso kwa uso na baby mama wa Diamond, Tanasha Donna.
Kitendo hicho cha Tanasha kuhudhuria shughuli hiyo kimelifanya tukio hilo kutrendi mno kwa sababu wengi hawakutarajia kwani ni mzazi mwenza wa hasimu wa King Kiba ambaye ni Diamond.
Hata hivyo, inafahamika kwamba, ukaribu wa wawili hao haukuanza hivi karibuni kwani kabla ya Tanasha kuzaa na Diamond alishafanya kazi na King Kiba akiwa kama video vixen kwenye Wimbo wa Nagharamia wa King Kiba na Christian Bella.
Pia taarifa za ndani zinasema kwamba, kuna wimbo wa pamoja wa Tanasha na Tommy Flavour ambaye ni msanii wa Lebo ya Kings Music iliyo chini ya King Kiba.