×

Orodha ya Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi linapenda kutangaza majina ya vijana wenye elimu ya shahada, stashahada, astashahada, kidato cha sita na kidato cha nne ambao walifanyiwa usaili na kuchaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Makao Makuu ya Polisi na Mikoani. Tarehe na utaratibu wa kuripoti Shule ya Polisi Moshi utatolewa na Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliofanyia usaili na watatakiwa kwenda na nauli zao kulingana na mahali wanapotoka hadi Moshi.

 

Kwa vijana walioomba nafasi za ajira kupitia vikosi ambavyo vipo chini ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kufanyiwa usaili Polisi Baracks Dar es Salaam, watatangaziwa siku ya kuripoti kupitia tovuti ya Polisi www.polisi.go.tz. Aidha, vijana wote wanaelekezwa kuwa siku ya kuripoti Shule ya Polisi Moshi wawe na vifaa vifuatavyo:

 

1. Cheti halisi cha kuzaliwa, vyeti halisi vya taaluma (original academic certificate); cheti cha kidato cha nne, kidato cha sita, astashahada, stashahada na shahada kwa ajili ya uhakiki.
2. Fedha taslimu Tsh. 50400/= kwa ajili ya kuingizwa kwenye mfumo wa bima ya afya kwa wasio na bima ya afya, na kwa wale wenye bima za afya waje na kadi zao.
3. Track suit ya rangi ya blue, T-shirt Nyeupe isiyo na maandishi, raba na bukta kwa ajili ya michezo.
4. Chandarua cheupe cha duara na sio cha pembe nne, shuka za light blue mbili, blanket lisilo na maua na pasi ya mkaa.
5. Wakiwa chuoni watatakiwa kununua vifaa vya usafi: kwanja, ndoo ndogo mbili na fagio la chelewa.
6. Fedha ya kujikimu.
Kwa mujibu wa kanuni za Shule ya Polisi Tanzania ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakaepatikana na simu atafukuzwa mafunzo mara moja. Shule itaelekeza utaratibu wa kupata mawasiliano.
Orodha ya vijana waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo ya awali ya kujiunga na Jeshi la Polisi nchini imeambatanishwa na tangazo hili.

 

Imetolewa na;
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,
S.L.P 961,
DODOMA.
19/10/2021

 

Orodha Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi 2021 

Leave a Comment