
RAPA wa Kimarekani anayetamba na albamu yake ya Expensive Pain, Robert Rihmeek Williams al-maarufu Meek Mill, ameweka wazi juu ya nia yake ya kutaka kustaafu muziki wa rap miaka michache ijayo.
Meek Mill alibainisha hayo wakati akifanyiwa mahojiano na mtangazi Speedy Morman kupitia kipindi chake cha Complex’s 360, ambapo alinukuliwa akisema kuwa; ameanza kurap tangu akiwa na miaka 23 hivyo hawezi kurap milele, lazima muda ukifika ataachana na muziki huo.
Staa huyo ameweka wazi juu ya mpango wake wa kuachia albamu nne au tano zaidi kabla hajaipa kisogo kazi hiyo ya muziki, Meek katika sehemu ya mahojiano yake alisikika akisema;
“I’ll still be rapping, but I ain’t gonna make that my priority of my day job.” (Nitaendelea kufanya kazi ya muziki kama rapa, lakini sitoifanya kazi ya muziki kama kazi yangu ya kila siku kama ilivyo kwa sasa).
Na Bakari Mahundu