×

Rais Samia Aongoza Kikao ha Baraza la Mawaziri

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 20, 2021 ameongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika lkulu Chamwino jijini Dodoma.

Rais Samia ameongoza kikao hicho ikiwa ni siku chache baada ya kufanya ziara ya kikazi katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Akiwa mkoani Kilimanjaro, Rais Samia alizindua barabara ya lami ya Sanya Juu-Elerai yenye urefu wa kilomita 32 na kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la wodi ya mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi.

Lakini kama hiyo haitoshi, Rais Samia akiwa mkoani Kilimanjaro, aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja la Rau ambalo lilisombwa na maji lakini mwisho alimalizia ziara yake kwa kufanya mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Chuo cha Ushirika pamoja na kushiriki Jubilei ya miaka 50 ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC).

Akiwa mkoani Arusha, Rais Samia alitembelea mradi wa maji uliopo Chekereni wilaya ya Arumeru pamoja na kuzindua mradi wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Engutoto kisha akazindua Kiwanda cha Nyama Elia Food Overseas LTD kilichopo wilayani Longido.

Leave a Comment