The House of Favourite Newspapers

Milionea Mdogo Zaidi Akamatwa

0

KIJANA milionea maarufu nchini Afrika Kusini, Sandile Shezi mwenye umri wa miaka 23 ambaye anajiita ‘Milionea Mwenye Umri Mdogo Zaidi’ nchini humo anashikiliwa na maofisa wa polisi kwa tuhuma za ulaghai.

 

Afisa wa Polisi katika eneo la Gauteng nchini humo, Mavela Masondo anasema kwamba Shezi alijipeleka mwenyewe polisi akiambatana na wakili wake baada ya polisi kumfungulia mashtaka hayo ya ulaghai.

 

‘Naweza kuthibitisha kwamba polisi walimkamata kijana huyo. Aliwasilishwa mbele ya hakimu wa eneo la Randburg siku ya Alhamisi ambapo alishtakiwa na mashtaka ya ulaghai’, alisema Masondo.

 

Shezi ambaye anayeishi katika Mji wa Durban anadaiwa kumlaghai mfanyabishara mwenzake wa Kampuni ya Global Forex Institute GFI na kumtapeli kiasi cha R500,000 ambazo ni sawa na $34,264 (Tsh milioni 78.978). ambapo polisi ilitoa kibali cha kumkamata kwake mapema mwezi huu.

 

Sandile Innocent Shezi amekuwa akijiita milionea mwenye umri mdogo zaidi , pamoja na mwenzake walianzisha biashara ya fedha za kigeni. GFI ni kampuni inayotoa mafunzo kwa watu kuhusu biashara ya fedha za kigeni ambapo pia huwafunza watu kuanzisha biashara zao.

 

Kijana huyo alianza ndoto yake ya kufanya biashara akiwa na umri mdogo ambapo alikuwa akichukua fedha kutoka kwa rafiki zake ili kufanya biashara.

Leave A Reply