
KUFUATIA Video chafu ya msanii kutoka Nigeria Tiwa Savage kuvuja kwenye mitandao, skendo hiyo imezidi kumtafuna msanii huyo mkubwa Afrika na kusababisha kupoteza dili 4 za makampuni makubwa tofauti.
Tiwa Savage amepoteza dili za kampuni makubwa ikiwemo ya mtandao wa simu ya GLO, Cadibury, Pampers na nyingine nyingi baada ya video hizo kusambaa zikimwonyesha akifanya mapenzi na mpenzi wake aitwaye Abolo Beckham ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa mafuta Kusini mwa Nigeria.
Muigizaji wa Nigeria ambaye anaishi Marekani, Gerogina Onuoha amedai kuwa Tiwa Savage ni msanii mzuri amebarikiwa lakini kutokana na hili inabidi aombe radhi.
Gerogina ameenda mbali zaidi na kutolea mfano mwanamitindo kutoka nchini Marekani, Kim Kardashian ambapo anadai aliandaa Tour ya kuomba radhi kwenye vituo vya habari na vipindi ili kuokoa brand yake aliyoitengeneza kwa zaidi ya miaka 15.

Staa huyo amesisitiza Tiwa Savage sio Msanii ambaye anaangaliwa Nigeria pekee ni Duniani anatakiwa kuomba radhi kwa hilo licha ya watu wengi kumtetea.
Kabla ya video hizo kusambaa, Tiwa wakati akihojiwa na New York’s Power 105.1 FM ya Marekani wiki chache zilizopita alidokeza kuwa ametumiwa picha za utupu akiwa na mpenzi wake, picha ambazo zilisambazwa kijana mmoja aliyeomba alipwe pesa ili asizisambaze jambo ambalo Tiwa alikataa kumpa pesa.
Tiwa alianza ku-date na Abolo mwenye utajiri unaokadiliwa kufikia dola milioni 3 hadi dola milioni 7 mara baada ya kuachana na mpenzi wake wa awali Obama Habeeb. Tiwa ambaye kwa sasa yupo London nhini Unhgereza na familia yake tangu sakata hili litokee, anakadiliwa kuwa na utajiri wa dola za Marekani milioni 12.
Nini maoni yako???