Mama wa Rapa Snoop Dogg Afariki Dunia
MAMA mzazi wa Rapper Snoop Dogg, aitwae Beverly Tate amefariki akiwa na umri wa miaka 70, chanzo cha kifo chake hakijatajwa lakini imeelezwa kwamba alilazwa Hospitali mwanzoni mwa mwaka huu.
July 25, mwaka huu Snoop Dogg aliwashukuru mashabiki wake kwa kumtakia afya njema mama yake ambaye alikuwa amelazwa hospitalini kufuatia hali mbaya ya kiafya
Tangu Mei 7 mwaka huu Snoop Dogg amekuwa akiposti mitandaoni picha tofauti akiwa na mama yake ambaye alikuwa mgonjwa.