×

Rais Samia Anakabidhiwa Kombe la COSAFA na Twiga Stars – Video

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Kombe la Ubingwa wa COSAFA kutoka kwa Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Twiga Stars.
“Pamoja na kwamba soka la wanawake limeanza miaka ya karibuni, lakini mafanikio yenu yameanza kuwatetemesha wanaume, timu ya wanawake imefanya vizuri mara kadhaa, lakini hakuna anayesimama kuwasifu, lakini mwanaume akishinda tu nusu fainali sifa zinapasua anga.
“Mawakala wa wachezaji wasemeeni wachezaji wetu, watangazeni ili wapate nafasi za kwenda kucheza nje ya nchi. TFF na BMT angalieni namna ya kuibua makocha wengi zaidi. Hakuna ubaya kocha wa kike kufundisha wanaume, mbona marefa wa kike wapo?
“Licha ya mafanikio yanayopatikana, lakini bado kuna changamoto nyingi katika kuendesha soka hapa nchini hususan soka la wanawake. Nilikuwa namwangalia mwanangu Fatma issa, hongera sana pamoja na hijabu yake lakini amecheza vizuri sana kwahiyo msitudharau tunaovaa Hijabu.

 

“Tunajipanga serikali ili kuanza kuweka vishikwambi (tablets) kwa ajili ya lugha za alama kwenye maeneo ambayo huduma za kijamii zinazotolewa ikiwemo mahospitalini…

 

“Tengenezeni makocha wengi zaidi, kwani kuna kosa kwa kocha mwanamke kufundisha timu za wanaume, mbona marefa wanawake wanachezesha mechi za wanaume?

“Nalipongeza sana Baraza la Sanaa kwa kuandaa mashindano ya Urembo na Utanashati, nikauliza kwani Mwanamke hawezi kuwa mtanashati? au kwakuwa kuna neno shati?”-Samia Suluhu, Rais wa Tanzania.


RAIS Samia Suluhu Hassan, leo Oktoba 27, amekabidhi kombe na kuwazawadia kuwapongeza wa timu ya Twiga Stars.. ⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/

Leave a Comment