
RAPA Willie Junior Maxwell II, maarufu kama Fetty Wap amekamatwa na Polisi wa FBI kwa tuhuma za dawa za kulevya.
Msanii huyo alikamatwa katika uwanja wa City Field huko Queens, ambapo tamasha la muziki la Rolling Loud lilifanyika siku ya Alhamisi Oktoba 28, 2021.
Msanii huyo na wenzake watano wanatuhumiwa kusafirisha, kusambaza na kuuza zaidi ya kilo 100 za dawa za kulevya aina ya heroini na fentanyl, katika kisiwa cha Long Island, na hivyo kuchangia kwa makusudi ugonjwa wa opioid.