
KESI ya uhujumu uchumi inayomhusisha Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wanaokabiliwa na mashtaka ya ugaidi, imeendelea tena leo Ijumaa, Oktoba 29, 2021 ikiendeshwa na Jaji Tiganga, katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ambapo shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka amepanda kizimbani kutoa ushahidi wake.
Jaji Tiganga aliingia katika mahakama hiyo saa 3: 50 asubuhi na kuanza kusikiliza ushahidi huo hadi saa 6:25 mchana kisha kuahirisha kwa muda na baadaye kuendelea tena.
Huu ni mtiririko wa kesi hiyo ilivyoendelea leo;
Jaji Joachim Tiganga ameingia na Waendesha mashtaka wanaanza kujitambulisha
Mawakili wa utetezi wakiongozwa na Peter Kibatala wanajitambulisha
Jaji anaanza Tiganga kuwaita washtakiwa kujiridhisha kama wote wapo.
Wakili wa Serikali Mwandamizi Robert Kidando: Shauri linakuja kusikilizwa leo tuna Shahidi mmoja na tuko tayari.
Kibatala: Nasi pia tuko tayari.
Jaji Tiganga anamtaka shahidi apande kizimbani na shahidi wa tatu, anapanda
Shahidi Hafidh Abdallah Momed, miaka 38, Askari Polisi, Muislam
Shahidi anaapa kiapo cha kutoa ushahidi wa kweli
Jaji anauliza kama kiapo kiko sawa kisha anamtaka karani amuongeze kuapa na karani anamuongoza.
Kidando: Shahidi ataongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hilla
Wakili Hilla anaanza kumuongoza
Naitwa Koplo Hafidh Hamisi, askari polisi Kinondoni, tangu mwaka 2003.
Kituo changu cha kazi ni Police Forensic Beurea, yaani Maabara ya uchunguzi wa kisayansi. Niko kitengo cha uchunguzi silaha na milipuko.
Kitengo changu kinahusika na uchunguzi silaha na milipuko niko kitengo hicho tangu 2004.
Majukumu yangu ni kuchunguza silaha zinazotuhumiwa kufanya uhalifu, kuchunguza risasi zinazotuhumiwa kufanya unalifu, kuchunguza maganda ya risasi mbalimbali, kuchunguza mahali palipo na mabomu. Kuandaa ripoti ya kitaalamu kuhusiana na kesi mbalimbali tunazozichunguza, kutoa ushahidi mahakamani.
Shahidi: Kuna uchunguzi aina mbili, moja ni physical examination ambapo tunapokea silaha mbalimbali zinazotuhumiwa kufanya uhalifu ili kutambua kama ni nzima na inafanya kazi, ambapo tunafanya uchunguz i wa awali yaani visual examination kama ina koki, magazine, kama skimu yake ni nzima (ya kuwekea risasi) kama kiwashio kinafanya kazi.
Jaji anamtaka shahidi atoe ufafanuzi wa maneno na kisha anaendelea.
Shahidi: Nitaangalia mtutu, nitaikoki kama inakoki
Shahidi: Aina ya pili ya uchunguzi unaitwa comparison examination ambapo nachukua ganda nililoletewa na ganda ambalo limepigwa ili kubaini ganda nililoletewa na bunduko niliyoletewa vinahusiana?
Tunatumia mtambo maalumu unaitwa computer microscope and digital camera forensic machine lelaeca 2004.
Kwenye risasi nitaangalia kiwashio, kama imegongwa, kama imegongwa tunasema hiyo siyo nzima maana imepigwa haikulipuka (missfired) yaani ni mbovu.
Kama haijagongwa ni nzima.
Pia tunaangalia gun powder. Tunaiangalia kama imeganda au iko sawa
Pia nitachunguza mapigo ya bunduki niliyoletewa na bunduki nyingine Kama yanqlingana.
Kwenye vichwa vya risasi tunaangalia michirizi maama risasi ikilipuka inaacha alama za kipekee na pia naangalia kitu kinaitwa twist. Pia tunaangalia count. Hivi ni vitu ambavyo vinsaidia kutambua silaha mbalimbali zinazofsnya uhalifu.
Kwenye mlipuko, tunakwenda eneo la tukio kujua kama ni local au industrial explosive.
Shahidi anaendelea
Mimi ni mtaalamu nimepata mafunzo ya ndani kwa askari wanobezi niliowakuta happy kwa miaka miwili. Hapo nilijifunza kuchunguza silaha na kuandaa ripoti.
Pia nilifanya kozi ya awali ya upelelezi, 2004 chuo cha Polisi Zanzibar ambako nilijifunza masuala ya upelelezi, kutunza bunduki, kupinga, kuchukua alama za vidole, kufungua na kufunga silaha, elimu ya vifaa mbalimbali vya silaha, kukusanya ushahidi eneo la tukio.
Nilipata kozi nyingine Chuo cha Polisi Moshi 2006 ambako nilijifunza masuala ya kufungua na kufunga silaha, kujua vifaa vyake na kutengeneza.
Baada ya historia ya mafunzo mbalimbali kwa nyakati na mahali tofaututofautu ndani na nje ya nchi na utaalamu, ambako alijifunza pia kuangalia majeraja na kujua upande alikokuwa mpigaji risasi na Kisha kuanza rasmi kazi ya uchunguzi mwaka 2010, sasa anaeleza utaraibu wa uchungu.
Kwanza mteja lazima awe na barua, ioneshe kosa, aeleze nini anataka wamfanyie. Pia anatakiwa kuwasilisha vielelezo husika. Barua na vielelezo hupokewa na afisa wa zamu. Akishapokea anafungua vielelezo husika baada ya kusoma barua ili jujiridhisha alichokiandika kwenye barua na akicholeta viko sahihi?
Naangalia usalama, maana ni silaha inaingia maabara. Baada ya hayo nitaingia maabara kuisajili na kuweka alama (kwenye vielelezo namba ikiwa ni pamoja na mwaka husika wa uchunguzi).Barua itapelekwa kwa incharge ili ajue nini kimeingia ofisini kwake na vielelezo vinapelekwa ghala la silaha.
Kuhusu kesi hii
Novemba 25, 2020, nilikuwa ofisini kwenye desk la kupokea vielelezo mbalimbali. Nakumbuma siku hiyo nilipokea vielelezo kutoka ofisi ya DCI ambavyo ni pistol namba A5344 ikiwa na magazine. Na nilipokea risasi 3. Risasi 3 za pistol.
Vielelezo hiyo alivileta askari PC Good luck kutoka ofiai ya DCI, pia aliwasilisha barua. Nilivi- lebel. Pisto niliipa alama Exh K1 nikaisajili kwa FB/158. Risasi nilizipabalama ya K2, K3 na K4. Nilizipa usajili wa 158.
Baada ya hapo nilirudi kwenye barua kujiridhisha wanataka nini niwafanyie. Walikuwa wanataka nifanye uchunguzi kutambua hiyo pistol na risasi ni nzima?
Baada ya hapo
Nili-minute na nikampelekea bosi kwamba leo nimepokea vielelezo kadhaa na vielelezo nikapeleka ghalani. Niliteuliwa mimi mwenyewe kufanya uchunguzi. Uchunguzi niliufanya kuanzia Novemba 25, 2020 wa awali.
Hatua ya kwanza nilipima ile bunduki kwa kifaa kinaitwa Gun Barow Gauge, kupima mtutu wa ile bunduki. Nikaona ni kweli iko sahihi. Nikatoa ile magazine yake, nikaingalia kama ni ya kwake nikaona ni ya kwake, nikaangalia spring ndani ya ile magazine nikaona Ni nzima, nikaangalia nyundo ya ile bastola kama ni strong, nikaona inagonga.
Baada ya hapo nikaenda kwenye trigger nikaipima kwa trigger tool nikabaini Ni nzima. Nikaikoki nikaona inakwenda vizuri. Kwenye risasi niliangalia pia nikabaini ni nzima.
Baada ya hatua hiyo ya visual examination nikaenda kwa uchunguzi wa kina ambapo nilichukua zile risasi mbili nilizoletewa nikaenda chumba maalum ambako kuna sehemu ya kupigia silaha mbalimbali. Nilikwenda na pistol na risasi 3.
Kile chumba kuna kifaa maalum kinaitwa tanki ambalo tunatumia kupata maganda ya risasi. Kuna maji ndani ya tenki hilo na nyavu hivyo ninapiga risasi humo ili nipate maganda na vichwa vya risasi. Hivyo kwenye tenki hilo nilipiga risasi 2 kati ya zile tatu nilizoletewa ili nijiridhishe sasa Kama hizo risasi ni nzima?
Nilipiga risasi za alama K2 na K4. Nilikwenda kuya-lebel maganda hayo mawili kwa alama T1 ambayo ilikuwa K2 na T2 ambayo ilikuwa K4. Baada ya hapo nikaenda kuandaa ripoti yangu (Ballistic examination report). Niliisaini na kupiga muhuri wa forensic.
Nilivifunga tena vielelezo hivyo nikasaini na kuvifunga kwa lakiri kisha nikavipeleka harmer (ghala la silaha) ripoti yangu nikaiweka kwa bahasha. Nilikuja kuchukuliwa Novemba 27, 2020 na afande Swila toka ofisi ya DCI na ni mimi niliyemkabidhi.
Nilimkabidhi ripoti yangu ya kiuchunguzi, possstol moja namba A5340 caliber 9 mim. Magazine na risasi moja nzima iliyobaki niliyokuwa nimei-lebel K3. Nikamkabdhi maganda mawili niliyoyalebel T1 na T2.
Tangu niliomkabidhi. Afande Swila vielelezo vile nilimuona jana ili aniletee vielelezo hivyo kwa ushahidi. Nikiviona nitavita bua kwa nembo ya ofisi, namba yangu ya Jeshi na majina yangu, signature yangu, muhuri wa ofisi.
Wakili Hilla anaiomba mahakama ili Shahidi atambue nyaraka mbalimbali na anamkabidhi Shahidi kablasha kisha anamtaka aieleze mahakama hicho ni nini.
Shahidi: Hii ni ripoti yangu niliyoiandaa kuhusiana na uchunguzi wa sila na risasi zile. Kisha Shahidi anaoneaha alama alizozitaja awali kama alama za kuitambua.
Shahidi anaiomba mahakama iipokee ripoti hiyo ipokewe kama kielelezo cha ushahidi wake.
Mawakili wa utetezi wanaikagua.
Wakili Nashon Nkungu, kwa mshtakiwa wa kwanza, John Mallya kwa mshtakiwa wa pili, Dickson Matata kwa mshtakiwa wa tatu na Peter Kibatala kwa mshtakiwa wa nne wansema kuwa hawana pingamizi ripoti hiyo kupokewa.
Jaji Tiganga: Mahakama inaipokea ripoti hii ya tarehe 26, Novemba 2020 kama kielelezo cha pili cha upande wa mashtaka. Nakuomba Shahidi usaidie kuisoma.
Shahidi anaanza kuisoma ripoti hiyo kilichomo.
Wakili Hilla anamuuliza maswali kumuongoza Shahidi kuelezea matokeo ya uchunguzi huo.
Shahidi: Kwa munibu wa uchunguzi nilibaini ya kwamba hii bastola ni nzima, inalipua risasi, hivyo inafanya kazi.
Shahidi: Kuhusu zile risasi 3 za pistol ile nazo ni nzima ni za pistol yenye caliber 9 mm.
Risasi na silaha vinahusiana yaani risasi hizo zilikuwa na pistol hiyo.
Kisha Shahidi anaelezea alama za kutambua vielelezo alivyovifunga baada ya kuvifanyia uchunguzi yaani bastola, risasi na maganda ya risasi. Mfuko wa nailoni mweupe imewekwa bastola. Mifuko mingine miwili ya nailoni, wa kwanza una risasi na wa pili una maganda mawili ya risasi na risasi zake.
Naiomba mahakama hii ipokee vielelezo hivi, kwanza bastola namba A5340 Caliber 9 mm na magazine model CZ100, risasi ya pistol caliber 99 mm. na mwisho maganda mawili ya bastola na vichwa vya risasi.
Upande wa Utetezi unaVikagua vielelezo hivyo, Kisha mawakili wa washtakiwa wote wanasem kuwa hawana pingamizi. Mahakama imevipokea vielelezo hivyo kuwa sehemu ya ushahidi wa Utetezi. Bastola hiyo, risasi na maganda yake.
Jaji Tiganga anavipa alama kama ifuatavyo.
Pistol kiel.n3, risasi moja ambayo haijatumika Kama kiel namba 4, maganda mawili ya risasi kama kielelezo namba 5. Bastola hiyo A5340 na magazine pamoja na risasi tatu kwa mujibu wa usahidi wa awali wa upande wa mashtaka ndio aliyokutwa nayo mshtakiwa wa pili Adamu Hassan Kasekwa baada ya kukamatwa Moshi na kupekuliwa.
Hivyo bastola aliyokutwa nayo mshtakiwa wa pili. Kasekwa imepokewa mahakamani pamoja na magazine na risasi zake. Sasa Wakili Hilla anampatia vielelezo hiyo shahidi ili avitolee ufafanuzi. Huku akimuongozea kwa maswali.
Wakili anaishika pistol hiyo na Jaji anamtania kuwa anatahadhari gani kuhusu usalama na kwamba halafu unamuelekezea Jaji, na hivyo kuibua vicheko kwa wasikilizaji mawakili wa pande zote na hata washtakiwa.
Shahidi sasa anaitolea ufafanuzi bastola hiyo kwa kuonesha sehemu zake na namba inavyofanya kazi kama alivyoelezea awali jinsi alivyofanya uchunguzi kujua kama ni nzima.
Shahidi mtaalamu wa silaha anaendelea kuichambua bastola ya mshtakiwa wa pili. Anaionesha na kuielezea mahakama sehemu mbalimbali za silaha na jinsi inavyofanyakazi, jinsi alivyofanya uchunguzi na matokeo aliyoyapata.
Upande wa mashtaka, wakili Hilla amemaliza kumuongoza Shahidi
Jaji: Upande wa utetezi?
Wakili Kibatala kwani anamtambulisha wakili Jeremiah Mtobesya ambaye alichelewa kwani alikuwa Mahakama ya Rufani na anaeleza kuwa ndiye atakayemujoji shahidi kwa niaba ya mshtakiwa wa kwanza.
Jaji Tiganga anamtaka Wakili Mtobesya ataje majina yake ili aingizwe kwenye kumbukumbu za mwenendo.
Jaji: Tumekwenda continuously na hatujapata break na sasa ni saa 6:25 nadhani ni vema tukapata break. Naahirisha mpaka saa 7:30, anaahirisha kesi hadi muda huo.