Rais Samia Aondoka Nchini Kuelekea Glasgow Scotland
Global Publishers October 30, 2021 0 Comments
SHARE THIS:
Rais Samia akisindikizwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokua akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30 Oktoba 2021 kuelekea Glasgow, Scotland kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na jitihada za kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa ili kupunguza joto Duniani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini leo tarehe 30 Oktoba 2021 kuelekea Glasgow, Scotland kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na jitihada za kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa ili kupunguza joto Duniani