
Canada inatambulishwa vyema kimataifa, baada ya muimbaji maarufu duniani kutokea nchini humo, @justinbieber kutajwa kwenye vipengele vingi kuliko msanii yeyote katika Tuzo za Peoples Choice 2021, ambazo zitafanyika Disemba 7 nchini California.
Upande wa Muziki, Bieber ametajwa kwenye vipengele vitano ambavyo ni: Mwanamuziki Bora wa Kiume, Wimbo wa Mwaka, Albamu ya Mwaka, Video Bora ya Mwaka pamoja na Korabo Bora ya Mwaka.
Upande wa ‘Pop Culture’ Justin Bieber ametajwa katika kipengele cha Mtu Maarufu katika Jamii pia ametajwa kwenye kipengele cha Pop Special kupitia ‘Tour’ yake ya muziki ya ‘Our World’ , Justin Bieber ametajwa kwenye vipengele 8!
Cc; @bakarimahundu