×

Jay Z Ajitoa Tena Instagram

BAADA ya jana kujiunga kwenye mtandao maarufu duniani wa Instagram nakupata followers million 2 ndani ya saa 24 akiweka post moja tu ya Movie yake mpya iliyotoka jana ya “The Harder They Fall”, nguli wa Hip Hop, Jay Z amejitoa tena kwenye mtandao huo muda mfupi tu baada ya ku-kremier Movie hiyo, huku ikitajwa kuwa kuingia kwake Insta ilikuwa ni kimkakati kuipromote movie hiyo!

 

Kwenye akaunti yake hiyo, Jay alikuwa amemfuata mtu mmoja pekee ambaye ni mke wake mwanamuziki maarufu Duniani Beyoncé Giselle Knowles-Carter.

 

Jay Z alijiunga na Instagram kwa mara ya kwanza Agosti 29, 2015, na kupost kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa marehemu Michael Jackson, lakini akaifuta programu hiyo masaa 14 tu baada ya kupata wafuasi 100,000 kwenye mtandao huo.

Leave a Comment