×

Rais Samia Afanya Ziara Coco Beach, Aongea na Wafanyabiashara -Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wafanyabiashara wadogowadogo katika eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza leo tarehe 04 Novemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na wafanyabiashara wadogowadogo katika eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza leo tarehe 04 Novemba 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Novemba 4, 2021 amefanya ziara ya kutembelea eneo la Ufukwe wa Bahari la Coco (Coco Beach) Jijini Dar es Salaam.

 

Rais Samia amewahakikishia Wafanyabiashara kwamba tayari Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu anazo Tsh. Bilioni 5 kwa ajili ya kuwakopesha Wamachinga ili ziwasaidie kukuza biashara zao.

 

“Niwaambie tunatafuta na fedha zaidi tumeongea na RC kwamba Jangwani pale napo tukajenge Soko kubwa la Wamachinga Vijana wetu tuwaweke pale, itapendeza Vijana wote tukiwa tumewapanga kwenye maeneo kuacha Mji wetu uko safi, salama”

 

“Soko letu la Kimataifa Kariakoo limeungua, hatuwezi kuliacha hivyo. Serikali imetafuta hela Bil.32 au 34 tunakwenda kulijenga soko la Kariakoo na tunalijenga kisasa, ramani ileile litaingiza Wafanyabiashara zaidi ya 2000.” amesema Rais Samia Suluhu Hassan.

Leave a Comment