The House of Favourite Newspapers

Mlokole Mainda anaswa!

0

IMG_3831
STAA mkongwe wa sinema za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ akikumbatiana na mwanaume huyo.

Musa mateja
STAA mkongwe wa sinema za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ ambaye ni mlokole wa Huduma ya Inuka Uangaze iliyopo kwenye Ukumbi wa Vatican City Hotel, Sinza jijini Dar, amenaswa laivu akiwa amegandana kimahaba na mwanaume hivyo kuibua minong’ono.

TUJIUNGE USHUANI MASAKI
Tukio hilo lililoshuhudiwa na gazeti hili lilijiri maeneo ya ushuani kwenye bustani zilizopo ndani ya Hoteli ya Double Tree, Masaki jijini Dar, juzikati ambapo kulikuwa na sherehe ya kuzaliwa ya mtoto wa mdogo wa Mainda, Rose Peter ‘Muna’.

MAINDA ATINGA ENEO LA TUKIO
Katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na baadhi ya mastaa na watoto wa mjini iliyonoga vilivyo, Mainda alishuhudiwa akifika eneo hilo la tukio majira ya saa 1:45 usiku akiwa peke yake ambapo awali alisalimiana na watu wachache kisha kujitwalia meza jirani kabisa na meza kuu.

Baada ya shughuli kukolea, Muna alimfuata Mainda na kumuomba wapige picha ya pamoja na mtoto wake kwa ajili ya kumbukumbu.

LULU NAYE ALIKUWEPO
Ili kuweka kumbukumbu zaidi, mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ naye aliwasogelea na kupiga nao picha ya pamoja huku waalikwa wakiendelea kula bata la nguvu lililoandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo.

MAINDA AENDELEA NA SALAMU
Hata hivyo, baada ya picha ya pamoja, Mainda aliendelea kusalimiana na watu wake ambao walionekana ‘kummisi’ hivyo kumchangamkia vya kutosha na kumshangaa alivyoadimika ikielezwa alikuwa akibanwa na shughuli za huduma ya Neno la Mungu.

IMG_3834

…..Wakizidi kugandana.

JAMAA ATOKEA, MAINDA AMRUKIA
Huku na huku wakati shughuli hiyo ikiendelea kwa watu kukata keki, kulishana, misosi na vinywaji, ghafla alitokea jamaa mmoja ambaye katika hali ya sintofahamu, Mainda alikurupuka na kwenda kumrukia kisha kugandana kwa dakika kadhaa wakionekana ‘kumisiana’ kwa muda mrefu.

WATUPIANA LAWAMA, MINONG’ONO YAIBUKA
Katika kugandana huko kimahaba, wawili hao walisikika wakilaumiana kutoonana na kutupana kwa siku nyingi hivyo kutumia muda huo kugandana ndipo ilipoibuka minong’ono kwamba, inakuwaje mlokole Mainda afanye mambo kama hayo hadharani?
“Jamani huyu si mlokole Mainda? Mbona kamgandia kifuani yule mwanaume? Kwanza huyu mwanaume ni nani wake?” alisikika akihoji mmoja wa waalikwa.

MAINDA AWAKA
Hata hivyo, Mainda aliposhtuka kuwa mwanahabari wetu alikuwa akimpiga picha baada ya kuona mwanga wa kamera, alianza kumuwakia huku akimtahadharisha jamaa huyo kuwa amuachie kwani sherehe ilikuwa imetibuka.

IMG_3835“Weee…(anataja jina la mwandishi wetu) sitaki udaku wako na ole wako nizione popote hizo picha. Mimi siku hizi siyo mtu wa aina hiyo,” alisikika Mainda wakati akijitoa mikononi kwa jamaa huyo aliyeonekana kutaka kuendelea kuonesha mahaba niue kwa mwanadada huyo.

Baada ya kumuona Mainda anakuwa mkali ilibidi kumuuliza jamaa huyo ni nani lakini hakuwa tayari kutoa ushirikiano kwa madai kwamba ina maana haruhusiwi kusalimiana na watu kwa kukumbatiana?

IJUMAA MZIGONI
Ilibidi Ijumaa liwafuatilie hatua kwa hatua ili kujua kama kuna chochote kilicho nyuma ya pazia lakini mpaka linaondoka eneo hilo halikufanikiwa kuambulia kitu.

MNYONGE MNYONGENI, HAKI YAKE MPENI
Pamoja na yote lakini Mainda ni mmoja wa mastaa wakubwa Bongo ambaye amedumu katika kumtumikia Mungu tangu akate shauri la kuokoka takriban miaka mitatu iliyopita ambapo amekuwa mstari wa mbele kuusimamia wokovu wake kwa dhati, akihudumu kwenye Nyumba ya Mungu kwa kufanya usafi asubuhi na jioni bila kukosa ibada.

Leave A Reply