×

Eti, Madalali Siyo Watu Wazuri?

 

WAZIRI wa Ardhi, William Lukuvi amewashukia madalali kote nchini na kuwaambia ni marufuku kuchukua kodi ya mwezi kwa wapangaji.

 

Hoja iliyopo mtaani hivi sasa ni kwamba, hao wapangaji watamudu kupata sehemu za kupanga kwa kutumia wenyeji wao?

 

Baadhi ya maoni yameonesha kuwa wengi hawawezi na kuweka mazigira hata kiasi ambacho wanatoa kwa madalali kimeambatana na hiyari ya mtu yenye lazima kimajukumu.

 

Ni kweli kodi hiyo inaumiza lakini wengi wanaeleza kuliko mtu aache kwenda kazini na kupekua mitaani kutafuta chumba au flemu ya biashara ni bora ampe dalali chake amtafutie chumba mambo yaishe.

Ni kama kumpatia ujira mteka maji nyumbani. Hapa weka kituo.

 

Upande wa pili wa maoni unaona ni heri madalali wakadhibitiwa hasa kutokana na tuhuma zinazowafanya wengine waonekane “kuwa na sumu.”

 

Sikia hii staili yao ya mfano: Kama mwenye nyumba akiwaambia anaiuza kwa milioni 30; dalali katika pitapita yake akampata wa kuinunua kwa shilingi milioni 70; fedha ile ya juu kwa maana milioni 40 yote ni yake.

 

Dalali haishii hapo yaani na ile ya mwezi ambayo ipo kwenye utaratibu; hataiacha na kujikuta ni kama yeye ndiyo kauza nyumba na mwenye nyumba kageuka dalali. Mbali na hiyo baadhi ya madalali wanahusishwa na michongo ya mijini; nikisema hivyo inaelewe.

 

Maisha yao yanatajwa yamekaa kimtandao zaidi na kuwafanya wajue kila kinachoendelea mitaani.

Sasa kwa hoja hizi hawa madalali ni kweli siyo watu wazuri? Linganisha na mahitaji ya jamii kwa watu hao hasa maeneo ya mijini.

 

Weka kisa chochote unachokifahamu kuhusu dalali na utoe maoni yako na kama unawachukulia poa tupia komenti ya kuwasifu.

@manyota_rich

Leave a Comment