
KONDE Boy Mjeshi au Teacher Harmonize ame shindwa kujizuia na kumwanika mrembo wake mpya kutoka Australia anayetajwa kwa jina moja la Briana.
Briana mwenye umri wa kati ya miaka 22 na 25, anatajwa kuwa ni mtu na nusu kwani ni modo mwenye umo matata na balozi wa kutangaza mavazi huku mambo mengine yakiwekwa chini ya kapeti.
Ishu ya Harmonize kuwa kwenye penzi na Briana zilianza kuvujishwa na Konde Boy mwenyewe kupitia Insta Story yake wikiendi iliyopita baada ya kuposti picha ya mkono wa mrembo huyo na akiwa ameshika picha yao wakiwa pamoja akiiambatanisha na maneno; “What a memory… (kumbukumbu iliyoje…)”
Kisha aliongeza ujumbe mwingine; “Finally I have the woman of my life…(hatimae nipo na mwanamke wa maisha yangu…)”