
Kampuni maarufu ya TAXI za mtandaoni ya UBER imesema itawaruhusu Watumiaji wake wa Ontario, Canada kuagiza bangi kupitia APP hiyo upande wa Uber Eats ambao hutumika kuagiza vyakula na vinywaji.
Ni zaidi ya miaka mitatu baada ya Canada kuhalalisha bangi kwa matumizi ya starehe ikiamini mpango huo utasaidia Watu wazima wa Canada kununua bangi salama, halali hivyo kusaidia kukabiliana na soko haramu la chinichini ambalo bado linachangia zaidi ya 40% ya mauzo yote ya bangi zisizo za matibabu kitaifa.

Uuzaji wa bangi nchini Canada utafikia dola bilioni 4 mnamo 2021 na unatabiriwa kukua hadi $ 6.7 bilioni mnamo 2026 kwa mujibu wa data kutoka kwa kampuni ya utafiti ya tasnia ya BDS Analytics.
Uber imeingia makubaliano na kampuni ya TOKYO SMOKE ambayo inamiliki maduka yauzayo bangi sehemu mbalimbali Nchini Canada ambapo Waagizaji watatakiwa kuthibitisha umri wao na kuchukua oda zao.