×

Man United ya Carrick Yapiga Mtu

Meneja wa muda wa Manchester United Michael Carrick ameanza kwa ushindi dhdi ya Villarreal ikiwa ni mechi yake ya kwanza tangu kukabidhiwa timu hiyo iliyokuwa chini ya Ole Gunnar Solskjaer.

 

Maabao ya Cristiano Ronaldo dakika ya 78 na Jadon Sancho dakika ya 90 yalitosha kuwapa furaha ya ushindi wa bao 2-0 vijana wa Carrick katika mechi yake yaka kwanza.

 

Aidha, Matumaini ya Barcelona ya kufikia katika hatua ya mchujo katika Champions League yako hatiani baada ya kutoka sare katika Nou Camp dhidi ya Benfica. Hivyo Barcelona analazimika kuhakikisha anamfunga Bayern ambaye ayakuwa nyumbani na kupiga dua kwa Benifica afungwe mechi yake ya mwisho ili kumpa nafasi Barca ya kusonga mbele.

 

Robert Lewandowski alishinda mechi tisa za mafanikio za Championi Ligi huku Bayern Munich wakiendela kushikilia rekodi ya ushindi wa 100% kwa ushini wa 2-1 katika kundi E dhidi ya Dynamo Kyiv.

 

Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel alisema kuwa klabu ilipata ” mafanikio mazuri” huku klabu hiyo ikisonga hadi katika kuwa miongoni mwa timu 16 za mwisho za Championi Ligi kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Juventus katika Stamford Bridge.

Leave a Comment