×

Ajioa Mwenyewe Kisa Umri Unaenda

Mwanamitindo wa Taifa la Brazil anayefahamika kwa jina la Cris Galera ambaye mwezi Septemba mwaka huu aliamua kufunga ndoa kwa kujioa mwenyewe kwa madai ya umri kumuacha akiwa hajapata wa kumuoa. ameamua kuivunja ndoa hiyo muda mfupi baada ya kupata mwanaume.

 

Kabla ya maamuzi hayo inadaiwa mwanamke huyo alikataa ofa kutoka mwanaume mmoja wa kiarabu aliyejitokeza na kutaka kumuoa baada ya kupata habari zake akiahidi kumlipa mahari ya zaidi ya shilingi za kitanzania Bilioni moja.

 

Hata hivyo mwanamke huyo alikataa akidai kuwa yeye sio bidhaa kuwa anauzwa na kuwa atakwenda kwa mwanaume mwingine aliyejitokeza na kuonesha kuwa anampenda kutoka katika moyo wake.

 

Alipoandaa hafla ya kujioa mwenyewe mbele ya kanisa moja huko Sao paul na picha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii akiwa katika hafla hiyo na mavazi ya bi harusi akiwa pamoja na maafiki zake ameendelea kuwa gumzo kila kukicha huko nchini kwao Brazil kiasi cha kuendelea kuwavutia wanaume wengi wakitaka kumuoa.

 

Alidai amechoshwa kutegemea furaha kutoka kwa wanaume ambao siku zote walikuwa wakimuangusha huku umri ukimuacha na ndipo alipoamua kujioa mwenyewe kabla ya kumpata mwanaume huyo mpya aliyeonesha nia ya kujioa.

 

“Niliyemkataa alinitumia ujumbe kuwa atalipa mahari ya dola laki tano za marekani kama mahari ya ndoa yetu endapo nitamkubali na kuivunja ndoa yangu niliyoifunga mwezi wa tisa” alisema membo huyo Galera.

 

Kupitia mtandao wa habari wa Daily star mrembo huyo amesema kwa sasa watu wasimshangae kwa kuvunja ndoa yake baada ya siku tisini na kwakuwa anatarajia kupata furaha kutoka kwa huyo aliyempata.

Leave a Comment