
MALKIA wa filamu za Bongo, Wema Sepetu amewatolea uvivu watu ambao wanamsema anaishi mbagala na kwenda mbali zaidi na Kutamani kujua kuna shida gani mtu kuishi mbagala, mwanadada huyo amefunguka hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha moja ya chombo cha habari .
Akizungumza na moja ya chombo cha habari, Wema amesema; “Tuseme ningekua naishi Mbagala kweli kwani watu ambao wanaishi Mbagala sio binadamu? au hawafai? au hawatakiwi? Kwa sababu Mbagala pia ni sehemu kama sehemu zingine.
“Wanaoishi Mbagala sio wanyama wala wadudu ni watu kama watu wengine na mimi nimesema nilikua nikiishi kule kwa sababu ya karma, kazi ndio ilinifanya niishi kule nimemaliza sina tena kitu kinacho nifanya niishi kule….” amesema Madam Wema.