Ommy Dimpoz afanikisha uzinduzi wa video yake
Ommy Dimpoz akiongea jambo wakati wa sherehe za uzinduzi wa video ya wimbo huo.
Mrembo aliyewahi kushiriki kwenye Big Brother Africa enzi hizo Abby akimpa kampani Ommy Dimpoz kwa kucheza kwenye uzinduzi huo.
Vanessa Mdee akiwa kwenye pozi mara baada ya kuwasili ukumbini hapo.
Wasanii wa Bongo Fleva Joh Makini na Ben Pol wakiwasili ukumbini hapo.
Baadhi ya warembo waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo wakiwa katika pozi.
Christian Bella akiimba kwenye uzinduzi huo
Mtangazaji wa Clouds FM Millard Ayo akimhoji jambo mmoja wa wasanii wa Bongo Fleva, Madee.
Ommy Dimpoz akimshukuru Bella wakati akiimba kama moja ya kumsapoti.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria ukumbini hapo wakifuatilia kwa makini zoezi la uzinduzi huo.
STAA wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, usiku wa kuamkia leo alifanikisha uzinduzi wa kichupa cha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Achia Body.
Uzinduzi huo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Akemi uliopo ndani ya jengo la Golden Jubilee Tower, ambapo ulihudhuriwa na baadhi ya wasanii wenzake kibao.
Wasanii waliojitokeza kumpa nguvu Ommy Dimpoz ni pamoja na Joh Makini, Ben Pol, Chege, Madee, Vanessa Mdee, Navy Kenzo Christian Bella na Mwana FA.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL