
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa,leo amezindua kongamano la kisayansi la kitaifa,kuhusu VVU na Ukimwi,katika ukumbi wa Mbeya Modern,Mkoani Mbeya,kwenye wiki ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi dunia,yatakayofanyika Disemba 1,mwaka huu Mkoani hapa, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Hassan Suluhu.

Katika ufunguzi wa kongamano hili,ambalo limeudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi,viongozi wa dini zote,limesisitiza hasa kila mmoja kupima kwa hiari kwaajili ya kutokomeza ugonjwa huu wa Ukimwi na kuondoa vikwazo vyote kwa kuzingatia usawa.