
Mahakama Kuu kanda ya Iringa iliyokaa kupitia kikao chake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe,imewahukumu washtakiwa wawili Mwapulise Mfikwa (29) na Manase Mhada (25) kunyongwa hadi kufa kwa kumuua Bi,Eva Merikion Mgaya (28) kwa kumpiga risasi mwaka 2015 nyumbani kwake huko kijiji cha Ihanga wilayani Njombe.