
MWANAMAMA ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na mwanamitindo wa kimataifa, Hamisa Hassan Mobeto anasema kuwa, yupo bize na mambo yake mengine na haweki mbele masuala ya kimapenzi hivyo baadhi ya watu
kudhani yupo singo, lakini ukweli ni kwamba watu wasijikanyage kwa sababu hayupo singo, ana uhusiano wake pambe tu.
Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Hamisa anasema kuwa, kuna wakati wa kuanza kuonesha uhusiano wake, lakini ukweli ni kwamba si kwa wakati huu kwa upande wake.
Anasema kwa sasa yupo kwenye harakati nyingine kabisa za kutafuta maisha, lakini siyo kwamba yuko singo na anafurahia uhusiano wake, bila kutaja yupo na mwanaume gani kwa sasa.
“Kuna watu wanapenda sana mtu akiwa na uhusiano, basi auweke bila sababu, lakini wakumbuke kuna kipindi mtu anafanya mambo yake ili maisha yaendelee, wanachopaswa kujua watu wasijikanyage sipo singo na maisha yanaendelea,” anasema Mobeto ambaye amezaa watoto wawili; mmoja na Diamond Platnumz na mwingine Majizzo.
STORI; IMELDA MTEMA, DAR