
WAKATI bado ngoma yake ya Bia Tamu ikiendelea kupenya kwenye masikio ya wengi na kusababisha vaibu kama lote, msanii Marioo amethibitisha kwamba hataki kupoa wala hapoi.
Bia Tamu inaendelea kufanya vizuri kwenye vituo vya redio ndani na nje ya Bongo. Pia, inafanya vizuri kwenye majukwaa ya kidijitali (digital platforms) mbalimbali duniani. Hata hivyo, pamoja na hayo, lakini tegemea kukutana na ngoma mpya kutoka kwa Marioo katika siku za karibuni kabla mwaka huu wa 2021 haujapinduka.
Hii ni baada ya Marioo kusema kuwa ngoma inakuja ‘soon’ akiwa amesmhirikisha msanii ambaye hakutaka kumtaja. Ishu hiyo imewafanya mashabiki wake kuamini kuwa huwenda kuna ngoma mpya nyingine inakuja kabla ya kuumaliza mwaka 2021.
STORI; SIFAEL PAUL, DAR