×

Saido, Mukoko Waapa Kuiua Simba

MASTAA wawili wa Yanga, Mrundi, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ na Mkongomani, Mukoko Tonombe, wamejiapiza kwa mashabiki kwamba watapambana kwa kadiri ya uwezo wao kupata matokeo ya ushindi kwenye mchezo
wao unaofuata dhidi ya Simba.

 

Watani hawa Simba na Yanga watakutana Desemba 11 huku Simba akimkaribisha mtani wake, Yanga kwenye
mchezo huo wa Ligi
Kuu Bara.

 

Kwenye mchezo uliopita walipokutana, Yanga iliwafunga Simba 1-0 kwenye Ngao ya Jamii.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Saido alisema: “Kikubwa ni kuomba uzima na afya kwa Mungu, kwa sababu nimejiandaa vizuri kuhakikisha yule Saido wa zamani ambaye mashabiki wa walimmisi anarudi na kasi mpya.

 

“Na huu ni mwanzo tu wa ligi, hivyo nitaendelea kufunga sana mabao mengi pale nitakapokuwa napata nafasi, kwa hiyo mashabiki wetu watarajie mambo mazuri kutoka kwetu.”


Kwa upande wake Mukoko,
alisema: “Mechi na Simba ni ngumu na tutapambana sana kuweza kupata alama tatu
muhimu kwenye mchezo huo
ili kuwapa furaha mashabiki zetu kama mchezo uliopita tulipokutana na mtani.

STORI: CAREEN OSCAR NA HAWA ABOUBAKARY, Dar

Leave a Comment