Baby J akiwapagawisha mashabiki.
….akiwaimbisha mashabiki.
Mabaunsa wakijaribu kuwatuliza vijana waliotaka kumvaa Baby J.
Baby Jay akiimba sambamba na Maromboso wa Yamoto Band.
Baada ya Baby Jay mwanamuziki aliyeibukia kupitia shindano la BSS, Juma Kayumba naye alivamia jukwaa na kuwapagawisha kwa ‘live band’ ambapo aligeuka koffi Olomide kwa muda na kupiga kibao cha Selfie ‘Ikotite’.
Muimbaji wa Taarabu, Zena Mohammed akiimba sambamba na Yamoto Band kibao alichoshirikiana na bendi hiyo ambacho ni kipya.
Yamoto wakiwa kazini katika kuburudisha kwenye usiku huo.
Kundi la Yamoto likiwajibika jukwaani.
Msanii wa kundi hilo almaarufu kwa jina la Chibu akiwapagawisha mashabiki.
Mdada kutoka pande za Zanzibar, Baby J usiku wa kuamkia leo alilipamba onesho la Yamoto Band na kuzua gumzo kufuatia bonge la burudani aliloporomosha kabla ya bendi hiyo kuwanogesha kwa burudani mashabiki waliofurika ukumbini hapo.
Katika onesho hilo lililofanyika kiwanja cha taifa cha burudani cha Dar Live kilichopo Mbagala – Zakhem jijini Dar, mashabiki walionekana kurukaruka kwa burudani hiyo mpaka majogoo.
(PICHA : RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY / GPL)