The House of Favourite Newspapers

Tonto Dikeh apewa Prado na mumewe kama zawadi ya Krismasi

0

Prado-2016-4

Toyota Prado

MSANII mwenye vituko kunako tasnia ya filamu, Nollywood, Tonto Dikeh Sikukuu ya Krismasi mwaka huu imekuwa nzuri kwake baada ya mumewe kipenzi, Olanrewaju Churchill kumkabidhi Prado nyeupe kama zawadi ya sikukuu.

Prado-2016-5Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tonto aliweka furaha yake kwa mashabiki kwa kutupia picha ya gari hilo na kumuita mumewe huyo KingKong.

“Ahsante kwa KingKong wangu kwa kunibariki gari hili ambalo ni jipya kabisa, Prado ya mwaka 2016. Mungu akubariki sana wewe mtu aka Mr. X, Mr. Bigchurch,” aliandika Tonto.Tonto na mumewe walifunga ndoa Agosti mwaka huu na bado hawajafanikiwa kuwa na mtoto.

(Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL)

Leave A Reply