
MKONGWE wa Manchester United, Rio Ferdinand ametaja timu tatu ambazo zinaweza kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2021/22.
Timu hizo ni pamoja na Manchester City, Liverpool na Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo la Ulaya.
Katika michuano hiyo ya Ulaya mpaka sasa timu kutoka ndani ya England zimetinga zote hatua ya 16 bora
kwenye UEFA.
Liverpool wao katika michuano hii wameweka rekodi kuwa timu ya kwanza ya England kushinda mechi zake zote sita hatua ya makundi.
Ferdinand amesema kuwa anazipa nafasi timu hizo za England kutokana na ubora wao kwa msimu huu.
Mkongwe huyo alisema: “Sio kama Bayern Munich inaweza kuzisumbua timu zetu za England (Liverpool, Chelsea na Man City) kwa sasa zina nguvu na zina makocha bora ambao wanawaeza kupambania hili
taji la UEFA.
“Ndiyo naona hizi timu zina nafasi kubwa ya kutwaa taji la UEFA kwa msimu huu. Timu kama Liverpool imekuwa kwenye kiwango cha juu na ikiweka rekodi bora ndani ya michuano hiyo ndiyo nirahisi kuipa nafasi.”