×

Uswizi Kupitisha Matumizi ya Kifaa cha Kujitoa Uhai

SERIKALI ya Uswizi ipo mbioni kuidhinisha matumizi ya kifaa maalum cha kusaijia kujitoa uhai kinachoitwa “Sarco Capsule”.

Kifaa hicho kimetengenezwa na shirika lisilo la Kimataifa la “Exit International” lenye makao yake makuu nchini Australia.


Takriban watu 1,300 walikufa kwa kusaidiwa kujiua nchini Uswizi kwa mwaka 2020 pekee hivyo kuidhinishwa kwa kifaa hicho kutarahisisha zaidi zoezi hilo.


Kwa mujibu wa mifumo ya kifaa hicho ni kuwa ukiingia utatakiwa kujibu maswali kadhaa na kurekodiwa kisha utabofya kitufe kwa ndani kuruhusu hewa ya Nitrojeni iingie na kukosa oksjeni ili upoteze fahamu baadae upoteze maisha ndani ya sekunde 30.


“Faida kwa mtu anayeitumia ni kwamba hawahitaji kupata ruhusa yoyote, hawahitaji daktari maalum kujaribu kuingiza sindano, na hawahitaji kupata dawa ngumu,” alisema Dr. Nitschke ambaye ndie mgunduzi wa kifaa hicho cha Sarco Capsule.


Watu husaidiwa kujiua kama familia zao zikikubaliana kutokana na mateso ya maumivu makali ya magonjwa kama kansa na yale yasiotibika.

Leave a Comment