×

Jaji Mkuu Awasajili Mawakili Wapya 313

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amekubali na kuwasajili mawakili wapya 313 katika sherehe ya 65 ya kuwakubali na kuwasajili mawakili wapya iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mawakili hao wanahusisha wanawake 170 na wanaume 143 ambao sasa wafanya idadi ya mawakili kufikia 10,749 kutoka 10,436 mwezi Juni mwaka huu katika orodha ya mawakili nchini.

Tukio hilo limefanyika leo Ijumaa, Desemba 10, 2021 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam ambapo Prof. Ibrahimu Juma amewataka Mawakili hao kuwa na nidhamu na kufikiria mbali zaidi kuliko kusubiri ajira.

“Maadili na viwango, hatupaswi kuwa na mawakili wasiokuwa na maadili, kosa moja la wakili linaweza kuzungushwa mitandaoni na kutuchafua na kuchukuliwa kama Tanzania nzima hatuna maadili. Endeleeni kupambana na mawakili vishoka.

“Na ukipiga mahesabu ya haraka haraka mliopo hapa 313 ni sawa na Sh bilioni 6 za uwekezaji kwenye elimu ya Sheria. Huo ni uwekezaji mkubwa sana,” amesema Prof. Juma.

 

Leave a Comment