×

Kufuru ya Pesa! Davido Ajinunulia Lamborghini ya Bil 1.26

IKIWA ni wiki chache tu baada ya kuchangiwa pesa na mashabiki zake mtandaoni kiasi cha Naira 250,000,000 (Tsh Bilioni (1.4) kwa na kuzipeleka kwenye vituo vya watu wenye uhitaji maalum, hatimaye mwanamuziki David Adeleke Adeleji maarufu Davido amejinunulia zawadi maalumu kwa ajili ya sherehe za sikukuu ya Krismasi.

Davido amenunua gari la kifahari aina ya Lamborghini Aventador lenye thamani ya $550,000 ambazo ni sawa na pesa za Kitanzania kiasi cha shilingi Bilioni 1.266.

Kabla ya hapo mwanzoni mwa mwaka 2021, Davido alifanikiwa kununua gari lingine la thamani aina ya Roll Royce Cullinan lenye thamani ya $500,000 ambazo ni sawa na Tsh bilioni 1.151.


Kutokana na thamani ya vitu anavyomiliki msanii huyo yakiwamo magari hayo ya kifahari, Davido anaendelea kujikita kwenye nafasi za juu miongoni mwa wasanii matajiri Barani Afrika.

Leave a Comment