
Rais Samia Suluhu Hassan amesema yupo tayari kukosolewa na kupokea maoni kutoka kwa viongozi wa vyama vya siasa pamoja na kusamehe na ili kufungua ukurasa mpya wa demokrasia nchini na kusisitiza kwamba viongozi wote wa kisiasa lazima wafanye shughuli zao kwa kuzingatia sheria.
Rais Samia ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa vyama vya siasa nchini ambao unalenga kujadili hali ya demokrasia ya vyama vingi nchini.
Kauli hiyo ya Rais Samia, imekuja baada ya kuombwa na mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini (TDC), Zitto Kabwe aliyemuomba amsamehe mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe ambaye kwa sasa anakabiliwa na mashitaka ya ugaidi na uhujumu uchumi.