The House of Favourite Newspapers

Fahamu aina za upungufu wa damu mwilini-2

0

TEST-ANEMIA-1024x576Katika makala ya wiki iliyopita tuliangazia tatizo la upungufu wa damu mwilini wengine huita Anaemia ambalo ni jina la jumla linalotumiwa kubainisha aina mbalimbali za upungufu wa damu mwilini.

Tukasema kiwango cha kawaida cha chembe nyekundu za damu (Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila milimita ya damu, zikiwa pungufu ya hapo mtu huyo anakuwa na tatizo la upungufu wa damu.

Tulitaja aina za upungufu wa damu kama vile Pernicious Anaemia na Aplastica Anaemia. Sasa endelea…

Sickle Cell Anaemia:
Ni aina nyingine ya upungufu wa damu ambao chembe nyekundu za damu huwa na muundo usio wa kawaida unaozuia na kuathiri mishipa midogo ya damu na hivyo kusababisha kuziba kwa mishipa hiyo ya damu.

DALILI ZA UPUNGUFU WA DAMU
Mtu mwenye tatizo la upungufu wa damu mara nyingi huwa amepauka mwili na viganja na kucha kuwa nyeupe na hujisikia kuchoka, udhaifu na huwa na mwendo kasi wa damu (yaani High Pulse Rate) na macho yake huwa meupe.

Dalili nyingine ni mgonjwa kuhisi kiu, kizunguzungu wakati akisimama, kuwa na mahangaiko ya moyo wakati akitumia nguvu kufanya jambo lolote, kuhema mfululizo na kupumua harakaharaka, mapigo ya moyo kwenda kwa kasi, kuhisi uchovu au hata kuishiwa kabisa na nguvu.

Dalili nyingine ni kusikia maumivu ya kifua pamoja na akili yake kushindwa kufikiri sawasawa, vilevile kuvimba kwa tumbo au sehemu za chini yake, kupoteza nguvu na macho kukosa nuru ya kuona vizuri.

VIPIMO NA MATIBABU
Uchunguzi wa wingi wa damu hufanyika kwa kupima kiasi cha mkusanyiko wa pamoja wa chembe nyekundu za damu kitaalamu huitwa Haemoglobin pamoja na kufanya kipimo kingine cha damu kijulikanacho kama Peripheral Smear.

Vipimo vingine vya maabara ni pamoja na kipimo cha kufahamu uwezo wa kuhifadhi madini ya chuma yaani Total Iron Binding Capacity (TIBC), kiasi cha Feritin katika damu pamoja na kiasi cha Folic Acid.

Aidha, katika mazingira mengine kipimo cha kuchukua sehemu ya supu ya mifupa na kuichunguza maabara yaani (Bone Marrow Biopsy) kinaweza kufanywa, japo si mara kwa mara.

Matibabu ya upungufu wa damu aina yoyote yanategemea aina ya upungufu wa damu unaomkabili mgonjwa.

Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya chuma kutokana na visababishi vya tatizo.
Licha ya hiyo, matibabu ya lishe yanaweza kutumika kwa ushauri wa daktari ingawa yanaweza yasitoshe hadi pale mgonjwa atakapoongezewa damu.

Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizo huweza kutumiwa na madaktari hospitalini sambamba na matibabu ya tatizo linalosababisha, iwapo mgonjwa yuko katika hali ya mahututi huweza kuongezewa damu.

Tatizo la upungufu wa damu ni tatizo la hatari sana endapo mwenye tatizo hilo atachelewa kupata matibabu mapema. Ukiona dalili hizo wahi kumuona daktari.

Leave A Reply