The House of Favourite Newspapers

Kukamatwa Wasomali, Wahabeshi Dar si salama

0

IMG_7619

Wakiwa katika hali ya sintofahamu.

Makongoro Oging’ na Issa Mnally, UWAZI
DAR ES SALAAM: Hatari! Kufuatia kukamatwa kwa wahamiaji haramu wapatao 42 raia wa Somalia na Ethiopia, Kijitonyama jijini Dar, hofu imetanda miongoni mwa raia ambao wanadai jiji hilo si salama.

Wahamiaji hao walikamatwa Jumapili iliyopita, katika nyumba namba 23, Kitalu 47 mali ya marehemu Mohamed Maganga ambayo kwa sasa inakaliwa na mjane, Salma Maganga akiwa pia mjumbe wa shina namba 23.IMG_7626

Wakiingizwa kwenye gari la polisi.

Kwa mujibu wa mjumbe huyo, vyumba ambavyo walikutwa wahamiaji hao alivipangisha kwa Amani Hamis, wiki nne zilizopita na hakujua kama kuna biashara hiyo inaendeshwa.

IMG_7652“Nami naishi hapa lakini nipo upande mwingine na siwezi kujua kinachoendelea upande huu. Nilishtuka polisi kufika hapa na kuniambia wamepata taarifa kuwa kuna watu si raia wanaishi hapa kwangu bila kibali,” alisema mjumbe huyo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mpakani ‘B’, Kata ya Kijitonyama, Balbo Kalinga amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola pale wanapoona jambo lisilo sahihi ama watu hatari kama hao.

IMG_7692

Mashuhuda wakiwa kwenye tukio hilo.

Wiki mbili zilizopita, gazeti hili liliripoti kukamatwa kwa Wasomali na Waethiopia 105 huko Tabata, Dar na hivyo kuzidisha hofu kuwa jiji hilo si salama kutokana na raia wa kigeni kuvuka mipaka na kuingia na kuishi kwenye makazi ya watu.

Leave A Reply