
Masuala ya uzazi yameonekana kumnogea msanii @malkiakaren baada ya kuweka wazi kutamani kupata watoto wanne pekee kwenye maisha yake.
Malkia Karen ameshea hilo kwenye ‘Insta Story’ yake baada ya shabiki kumuuliza kwamba ni watoto wangapi amemuomba mungu amjaalie.
Karen akajibu ni watoto wanne pekee, mpaka sasa msanii huyo ana mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Celeb.