
MALKIA Karen ni msanii mwingine mkali wa kike kunako Bongo Fleva ambaye ambaye ameibua gumzo hivi karibuni baada ya kudaiwa kuzaa mtoto na Diamond Platnumz.
Kwa mara ya kwanza, Karen amevunja ukimya juu ya ishu hiyo akisema kuwa, hana mtoto na Diamond kama watu wanavyosema.
Karen amesema hana mtoto na Diamond hivyo watu waache kumhukumu vibaya.
“Ni kweli umezaa na Diamond?” mmoja wa mashabiki wake amemuuliza Karen.
“Hapana,” Amejibu Karen.
Hivi karibuni Karen alijaaliwa mtoto wake wa kwanza huku vyanzo vya ndani vikibainisha kuwa, mtoto huyo amezaa na jamaa ambaye siyo maarufu na hapendi kuwekwa mitandaoni kwa kuwa ni mfanyakazi katika idara nyeti serikalini.