
SERIKALI imesema itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa Mabasi yote ambayo yanapuuza agizo la Serikali na kuendelea kupandisha nauli msimu huu wa sikukuu ambapo kuanzia leo atakayepandisha nauli atatozwa faini ya Tsh. 500,000.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara amesema hayo leo alipotembelea Stendi Kuu ya Mbezi Dar es salaam na kusema hakuna yeyote anaeruhusiwa kupandisha nauli tofauti na ile iliyopangwa na LATRA.
Waitara alitembelea pia katika Stendi hiyo juzi na kutoa maagizo ya nauli kutopandishwa lakini amesema bado Kumekuwa na kupuuzia kwa agizo lake.