×

Ruby Afunguka Kurudiana na Kusah

MSANII wa Bongo Fleva, Ruby amesema suala la yeye kurudiana na mpenzi wake wa zamani, Kusah ambaye kwa sasa yupo na Aunty Ezekiel ni jambo lisilowezekana.

 

Ruby ambaye alikuwa amejaliwa kupata mtoto mmoja Kusah, alidai kuachana kwao ni kwamba Kusah alikuwa akimpiga mara kwa mara.

“Hizo ni ndoto za Firauni, zishindwe kwa jina la Yesu” Ruby amemjibu shabiki aliyetaka staa huyo kurudiana na Kusah.

 

Ikumbukwe kipindi cha mahusiano yao, Ruby na Kusah walifanikiwa kutoa nyimbo mbili pamoja ‘Chelewa na Nadondosha’ na kupata mapokezi makubwa.

Leave a Comment