×

Simbachawene Aagiza Polisi Kumhoji Askofu Mwingira – Video

WAZIRI wa Mambo ya Ndani George Simbachawene, amemtaka Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, kumtafuta na kumhoji Askofu wa Kanisa la Efatha, Josephat Mwingira aliyedai amenusurika kuuawa mara tatu na watu wa serikali ili kusaidia kupata ukweli zaidi wa tuhuma hizo nzito alizozitoa.

 

Simbachawene ameyasema hayo leo Jumatatu Desemba 27, 2021 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu masuala mbalimbali.

 

Hatua hiyo ya Waziri Simbachawene imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii zikimnukuu Askofu Mwingira akutoa tuhuma mbalimbali ikiwemo kutishiwa maisha na mali zake kuteketezwa shambani kwake.

 

“Nimeona tuhuma zimetamkwa na Askofu Mwingira, tunaendelea kufuatilia, zinapotolewa na kiongozi maarufu, tunapata shida, kwa nini hatoi taarifa, mpaka yametokea, unakaa kimya, unasubiri Krisimasi ndio unasema, kama ni kweli, tutahitaji atusaidie atupe ukweli,” amesema Simbachawene.

Leave a Comment