×

Kifaa Kipya Yanga Kutua Dar Kesho

WINGA wa TP Mazembe, Chico Usindi Wakubanza, tayari ameshaaga huko kwao DR Congo na kujiandaa kwa safari
ya kutua Tanzania
kuanza maisha mapya ndani ya kikosi cha Yanga.


Kifaa hicho
kimemalizana na Yanga ambapo atajiunga na klabu hiyo kwa mkopo wa muda mrefu wenye kipengele cha kubaki klabuni hapo moja kwa moja au kuuzwa.


Akizungumza na Spoti Xtra,
Ushindi aliweka wazi kuwa safari yake ya kutoka DR Congo inaanza rasmi leo Jumanne usiku, huku akitarajiwa kufika nchini kesho Jumatano tayari kwa ajili ya kujiunga na Yanga ambayo ni timu yake mpya.

 

“Safari Yangu inaanza rasmi Jumanne ambapo nitatoka usiku huku DR Congo na kisha nitafika Tanzania Jumatano (kesho) tayari kwa ajili ya kujiunga rasmi na Yanga.


“Tayari uongozi wa TP
Mazembe na marafiki zangu wanafahamu hili na nimeshawaaga na wamenipatia baraka zote, hivyo natarajia pia kupata mapokezi mazuri nikiwa Tanzania kwa ajili ya kuipigania Yanga,” alisema mchezaji huyo.

MARCO MZUMBE, Dar

Leave a Comment