×

Pablo Ataja Sababu za Ajibu Kuondoka Simba

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco ameweka wazi kuwa sababu kubwa ya timu hiyo kuachana na baadhi ya
mastaa akiwemo kiungo, Ibrahim
Ajibu aliyejiunga na Azam ni kuwaambia wazi kuwa hawakuwa na nafasi ndani ya kikosi chake.


Simba ilitangaza rasmi juzi
Alhamisi kusitisha mkataba na Ajibu kwa kile kilichoelezwa kuwa ni makubaliano ya pande zotembili, ambapo nyota huyo tayari ametangazwa kusaini mwaka mmoja ndani ya kikosi cha Azam.

 


Pamoja ana Ajibu, Simba kwenye
dirisha hili la usajili inatarajia kuachana na nyota watatu wa kikosi hicho wakiwemo winga, Duncan Nyoni na kipa Jeremiah Kisubi ambao wanatarajiwa kutolewa kwa mkopo ili kuboresha kikosi chao na kusajili nyota wengine.


Akizungumza na Championi
Jumamosi, kocha Pablo alisema: “Ni kweli tulifikia muafaka wa kuachana na baadhi ya wachezaji wa kikosi chetu na hii ni kutokana na ukweli kuwa nilikaa na wachezaji hao na kuwaweka wazi kuwa wasingekuwa na nafasi kwenye kikosi changu.


“Lakini pia baadhi yao
walishindwa kufikia matarajio yao binafsi na ya klabu, hivyo kama wanadamu ni lazima pia tuangalie faida ya pande zote mbili na ndiyo sababu ya kuachana nao.”

Stori: Joel Thomas, Dar es Salaam

Leave a Comment